0

Ndege ya Ukraine yatua Zanzibar na watalii 215

Mon, 26 Oct 2020 Source: habarileo.co.tz

NDEGE ya Shirika la ndege la Sky up la Ukraine imewasili visiwani hapa ikiwa na watalii 215.

Ndege hiyo ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume . Kamishna wa Kamisheni ya utalii Zanzibar, Khamis Mbetto alisema hayo ni mafanikio makubwa tangu Zanzibar kuruhusu shughuli za utalii baada ya kumalizika kwa ugonjwa wa covid-19Juni 6 mwaka 2020.

Alisema ndege nyingine kutoka Urusi inatarajiwa kuwasili Zanzibar wiki ijayo . Ofisa mwandamizi kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Haji Ali alisema wamejipanga vizuri kupokea watalii wanaowasili nchini huku tahadhari ya virusi vya corona imechukuliwa.

Alisema wanatarajia kupokea ndege zaidi katika kipindi cha wiki mbili zijazo ambapo watalii watatembelea maeneo ya visiwa vya Unguja na kujionea mandhari pamoja na historia ya magofu ya kale.

‘’Tunatarajia kupokea watalii wengi zaidi pamoja na ujio wa ndege kubwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo, hatua ambayo itafungua masoko ya utalii pamoja na bidhaa mbalimbali ndani ya visiwa,”alisema

Chanzo: habarileo.co.tz