0

Mzuka umehamia CRDB Taifa Cup

Mzuka umehamia CRDB Taifa Cup

Thu, 12 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By Mwanahiba Richard na Matereka Jalilu Mashindano ya Kombe la Taifa kwa mchezo wa mpira wa kikapu yajulikano kama CRDB Taifa Cup yanaanza leo jijini Dodoma na yatashirikisha timu 36 za wanaume na wanawake.

Mashindano hayo yaliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), hufanyika kila mwaka na kwa mikoa tofauti na mwaka jana yalifanyika mkoani Simiyu.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na CRDB, ambao wametoa kiasi cha Sh200 milioni, ambazo zitatumika katika shughuli zote za mashindano hayo ikiwemo zawadi kwa washindi huku, Sh50 milioni ikitengwa kwa ajili ya programu maalumu kwa vijana chini ya miaka 18.

Vijana hao watapa ufadhili wa kusoma nje ya nchi na watapatikana kupitia mashindano hayo baada ya TBF kuzitaka timu zote kusajili baadhi ya wachezaji watatun wenye miaka chini ya 18 na watakaoonyesha kiwango bora watanufaika na ufadhili huo.

Mashindano hayo yataanza rasmi leo, lakini kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano, Haleluya Kavalambi, ratiba imebadilika hivyo ufungizi rasmi utafanyika kesho baada ya shughuli ya Rais John Pombe Magufuli kumaliza kuhutubia nchi leo.

Haleluya alisema kwa mabadiliko hayo, mechi ambazo zilipangwa kuchezwa leo zitachezwa kesho na zile za kesho zinarudi nyuma, ambayo ni michezo miwili ya ufunguzi.

Chanzo: Mwanaspoti