0

Kituo kipya cha mabasi Mbezi Luis kuanza kutumika Novemba 25

Kituo kipya cha mabasi Mbezi Luis kuanza kutumika Novemba 25

Mon, 9 Nov 2020 Source: HabariLeo

Kituo kipya cha mabasi ya mikoani kinachojengwa Mbezi Luis kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi Novemba 30 mwaka huu baada ya ujenzi wake kufikia asilimia 90.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema kabla ya kuanza kutumika kwa kituo hicho yatafanyika majaribio ya kwanza Novemba 25.

Kunenge amesema maombi kwa ajili ya uendeshaji wa fursa mbalimbali zinazopatikana katika kituo hicho yamefunguliwa na mwisho wa kupokea maomba hayo ni Novemba 25 mwaka huu.

Alitaja fursa zinazopatikana katika kituo hicho ni fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, ‘supermarket’ na ofisi za kukata tiketi.

Chanzo: HabariLeo