0

Jovitha anavyozalisha sabuni kwa kutumia vyakula

Jovitha anavyozalisha sabuni kwa kutumia vyakula

Thu, 8 Oct 2020 Source: HabariLeo

ALIANZA kama mjasiriamali wa kutengeneza sabuni kwa kutumia malighafi ambazo wengi wanazitumia.

Lakini sasa, kinachomtofautisha na wajasiriamali wengine katika sekta hiyo ni kubuni utengenezaji wa sabuni za vipande na za maji kwa kutumia viungo vya chakula au matunda mbalimbali bila kuweka kemikali.

Huyu si mwingine bali Jovitha Mavoa, mkazi wa Kibaha mkoani Pwani anayezipa bidhaa zake hizo jina la Jonoma Products.

Kutokana na sabuni zake kutumia vyakula vyenye viinilishe mbalimbali, Jovitha anaamini kwamba sabuni hizo zinapotumika kwa ajili ya kuogea huwa ni kinga ya ngozi dhidi ya magonjwa mbalimbali, hutibu magonjwa lakini kubwa zaidi ni kutunza ngozi ya mtumiaji.

Anasema anatengeneza sabuni kwa kutumia liwa, ubuyu, nyanya, mchaichai, tangawizi, mchele, mbilimbi, kitunguu swaumu, mkaratusi na mazao mengine.

Malighafi nyingine anazotumia katika kuchanganya ni mafuta ya binzari, manjano, mafuta ya mawese, mafuta ya ng’ombe, mafuta ya nazi, mafuta ya kondoo na mbegu za chikichi maarufu kama mise.

Anasema kilichomsukuma kubuni sabuni hizo ni kutokana na wateja wake ambao walikuwa akiwatengenezea sabuni za maji na za vipande kwa kutumia malighafi zenye kemikali kisha wakawa wanamuuliza kama anaweza kutengeneza tatizo la viwavijeshi vamizi na hawajui la kufanya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Seliani mkoani Arusha, Dk Joseph Ndunguru amenukuliwa akisema kwamba viwavijeshi vamizi wameleta hasara kubwa katika uzalishaji wa mazao mbalimbali hasa zao la mahindi ambalo hutegemewa na watu takribani milioni 200 kwa chakula katika Bara la Afrika.

Anasema Kituo cha Kimataifa cha Kilimo na Bioteknolojia (CABI), kimekadiria hasara itokanayo na viwavijeshi vamizi ya wastani wa tani 2,365,000 sawa na dola za Marekami kati ya milioni 381 hadi 948 nchini Tanzania pekee na dola milioni 6,312 kwa bara zima la Afrika kwa kipindi cha mwaka 2017.

Madhara mengine yanayosababishwa na kiwavijeshi vamizi huyo katika ngazi ya kaya ni kuleta upungufu wa kipato kwa kuwa mazao mengi yanashambuliwa kabla ya kukomaa, anasema Dk Ndunguru.

Anasema mitaji ya biashara pia hukata kutokana na kutofikia lengo wakati wa kuvuna, huku wakisababisha pia uhaba wa chakula kutokana na mazao kushambuliwa yakiwa yangali shambani.

Vile vile kiwavijeshi vamizi huyo, husababisha ongezeko la gharama katika biashara ya mazao ya kimataifa kwa vile nchi mbalimbali inabidi zichukue hatua za ziada za ukaguzi wa mazao ambazo huleta ongezeko la gharama.

Mbinu ya kisayansi inayoelezwa na Dk Ndunguru katika kumdhibiti mdudu huyo ni kufanya utafiti wa viwavijeshi vamizi kwa kutumia vipimo vya DNA.

Anasema hatua hiyo itasaidia kubaini makundi ama jamii mbalimbali za viwavi jeshi vamizi ili kuwa na uchaguzi sahihi wa aina ya viuatilifu vya kuangamiza makundi na jamii hizo kwa ukamilifu.

Anasema mbinu nyingine muhimu ni matumizi ya mbegu zenye kustahimili mashambulizi ya viwavi jeshi vamizi.

Mbegu hizo ni kama zile za Mradi wa Mahindi yanayostahimili Ukame (Wema). Dk Ndunguru anataja njia nyingine matumizi ya udhibiti husishi ikiwemo kukagua mashamba mara kwa mara ili kubaini uwepo wa wadudu hao na kuzingatia usafi wa mashamba.

Anasema hadi kufikia Juni 2017 nchi 19 zilikuwa zimevamiwa na kiwavijeshi huyo. Anasema nchi hizo zimekuwa zikichukua hatua mbalimbali za kumdhibiti mdudu huyo kwa njia mbalimbali.

Jovitha anavyozalisha sabuni kwa kutumia vyakula ambazo zitakazotokana na vyakula.

Anasema waliokuwa wakimuuliza swali hilo mara kwa mara ni wale waliokuwa wanashindwa kutumia bidhaa zinazotengenezwa viwandani kutokana na kuwaletea madhara yanayosababishwa na kemikali zinazotumika na kushauriwa na madaktari kutumia sabuni zisizo na kemikali.

Mbali na sabuni, Jovitha pia anatengeneza mafuta ya kujipaka yatokanayo na nazi, vicks, mafuta ya nyonyo, mafuta kwa ajili ya kukandia mwili (massage) na mafuta kwa ajili ya nywele.

“Nilipoanza kutengeneza sabuni kwa kutumia vyakula watu wengi wamezifurahia kwani hazina madhara yoyote kwa mtumiaji tofauti na za viwandani.

Ukweli ni kwamba zile za viwandani ambazo hudaiwa kuwa na viungo, siyo viungo halisi bali wanaweka tu ladha ya viungo lakini mimi natengeneza kwa viungo vyenyewe,” anajigamba Jovitha.

Mwanamke huyo anasema bidhaa zake zimekuwa pia zikiwasaidia akina mama ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta mafuta au sabuni ambazo zinafanya ngozi zao kuwa laini na za kuvutia.

Bidhaa nyingine anazotengeneza kutegemea uhitaji ni sabuni za chooni kwa kutumia aloevera, nyanya na pilipili. Jovitha anafafanua kwamba bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia vitunguu swaumu zinasaidia kuondoa maradhi ya ngozi na majeraha na kwamba ni kinga ya ngozi dhidi ya maradhi.

Anasema upande wa mbilimbi ina vitamini C inayosaidia kuondoa vipele, chunusi na makovu. “Mchele hung’arisha ngozi ya mtumiaji na kuifanya isiwe na mafuta mengi na hivyo mtumiaji halazimiki kutumia lotion wakati riwa inaposugua usoni husaidia kuung’arisha ngozi ya uso.

Nyanya ina faida ya kuifanya ngozi isijikunjekunje kutokana na kuwa na vitamin E,” anasema. Anasema bidhaa zake amekuwa akizitengeneza kwa mfumo wa kisasa kwa kuziweka kwenye maboksi au chupa sahihi.

Anasema mafunzo ya kutengeneza sabuni aliyapata kupitia Shirika la Kusaidia Viwanda Vidogo (Sido).

Kwa siku moja, Jovitha anasema ana uwezo wa kutengenza vipande vya sabuni 400 na kwamba bidhaa zake zina nembo na alama muhimu misimbomilia (barcode), zimekaguliwa na mkemia mkuu na sasa yuko kwenye mchakato wa kuwa na nembo ya ubora wa bidhaa kutoka Shirika la Viwango (TBS).

Kwa upande wa mafanikio anasema ameweza kufundisha watu 450 katika wilaya ya Kibaha na huku pia akifundisha watu takribani 200 Kipunguni Dar es Salaam kuhusu utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni.

Anasema baadhi ya bidhaa zake anaziuza katika mikoa ya Tanga, Mbeya na Morogoro na ameshahudhuria maonesho mbalimbali kwenye mikoa ya Mbeya, Tabora, Mwanza, Arusha, Moshi, Tanga, Morogoro, Mtwara, Lindi na Zanzibar. Kwa upande wa nje ya nchi alishashiriki maonesho yaliyofanyika Zambia.

Mafanikio mengine anasema ameweza kujenga nyumba ya kuishi na kununua pia eneo lenye ukubwa wa ekari 10 huko eneo la Michungwani mkoani Tanga.

Anasema malengo yake ni kujenga kiwanda cha kufanyia shughuli zake katika eneo hilo lililoko Tanga, lakini kwa sasa anatengenezea bidhaa zake sebuleni mwake.

Aidha anasema yeye na wajasiriamali wenzake wamepewa eneo na Halmashauri ya Mji wa Kibaha ambapo wako zaidi ya wanawake 40 kwa ajili ya kuuza bidhaa zao mbalimbali.

“Wakati wa kipindi cha ugonjwa wa corona kwangu ilikuwa fursa kwani nilitengeneza vitakasa mikono vingi na sabuni na biashara ilikuwa kubwa,” anasema na kuongeza kwamba kutokana na mauzo ya uhakika kipindi cha corona alifanikiwa kuongeza mtaji wake.

Kuhusu changamoto anazokuta nazo Jovitha anasema ni pamoja na malighafi kupoteza ubora kutokana mahala zinakotoka na zingine au kukaa kwa muda mrefu.

Changamoto nyingine anasema ni ukosefu wa soko kutokana na wananchi wengi kutojua uwepo wake na pia uhaba wa mtaji. Kupata muda wa kutosha wa kuhudumia familia huku pia akizalisha bidhaa zake anasema ni changamoto nyingine anayopambana nayo.

“Lakini ninamshukuru mume wangu amekuwa akiniunga sana mkono katika shughuli zangu,” anasema. Akielezea kidogo kuhusu alivyoanza shughuli za ujasiriamali, Jovitha anasema alianza kwa kuuza mboga, akizitoa Kibaha na kuzipeleka Kariakoo mwaka 1993.

Anasema kuna wakati, kutegemea upatikanaji wa mboga alilazimika yeye na wafanyabiashara wenzake kufuata mboga Uyole, Mbeya.

Anasema mume wake aliwahi kuondoka nyumbani kwenda Msumbiji bila kuaga, safari ambayo ilimfikisha Afrika Kusini kutafuta maisha na kusababisha maisha yake kuwa magumu sana.

Katika kipindi hicho cha miaka mitatu anasema alilazimika pia kuuza na maandazi na kupika chakula kama mama lishe kwenye Shule ya Sekondari ya Kibaha.

Anasema baadaye mumewe alirejea, akajaribu kutafuta maisha Tunduru napo hayakuwa mazuri na kisha wakaamua kwenda kuishi Buguruni Dar es Salaam kabla ya kurudi Kibaha.

Harakati alizopitia akiwa Dar es Salaam, anasema ni pamoja na kuuza maji ya kwenye mifuko ya nailoni kwa wakati ule yalikuwa maarufu maji ya Kandoro.

Jovitha anamshukuru pia rafiki yake kutoka Zanzibar aliyeboresha ujuzi wake wa kutengeneza sabuni kwa kutumia vyakula na hii ikiwa ni mwaka 2017.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) mkoani Pwani, Abdallah Ndauka anasema wanashirikiana vyema na mjasiriamali huyo katika masuala mbalimbali kwani Jovitha pia ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo upande wa wanawake.

Mmoja ya wajasiriamali ambaye amenufaika kutokana na mafunzo ya Jovitha ni Said Ngunde ambaye naye anatengeneza bidhaa kama zake.

Ngunde anasema hatua hiyo imesaidia kubadilishia maisha yake ambapo anashirikiana na mke wake kuzalisha sabuni na mafuta.

Chanzo: HabariLeo