0

DRONE PICTURES: Stand mpya ya mabasi Mbezi Luis "Majaribio November 25"

DRONE PICTURES: Stand mpya ya mabasi Mbezi Luis "Majaribio November 25"

Wed, 18 Nov 2020 Source: Millard Ayo

Kutoka Mbezi Louis Dar Es Salaam, hii ni Drone Video ya Stand Mpya ya Kisasa ya Mabasi ya Mikoani iliyogharimu Tsh. Bilioni 71 ikiwa na uwezo wa kuruhusu Mabasi zaidi ya 1000 na Taxi 280 kupark, agizo la Rais Magufuli la Stand kukamilika kwa baraka limefanyiwa kazi na sasa kazi zinafanyika usiku na mchana.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Aboubakar Kunenge Ujenzi wa Stand hii umefikia 90% na itaanza majaribio ya Kwanza November 25 na kuanza kutumika rasmi November 30 mwaka huu.

RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye stand hii ikiwemo fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, supermarket, ofisi za kukata tiketi na hotel ambapo zoezi la kutuma maombi limeanza November 09 hadi November 25.

NJIWA WANALIPA! MWINGINE TENA AUZWA KWA ZAIDI YA TSH. BILIONI 3, “AMEVUNJA REKODI YA DUNIA”

Chanzo: Millard Ayo