0

Billionea Laizer aibuka na jipya baada ya CCTV Camera mirerani "tulikuwa na wasiwasi"

Billionea Laizer aibuka na jipya baada ya CCTV Camera mirerani "tulikuwa na wasiwasi"

Thu, 19 Nov 2020 Source: Millard Ayo

Baada yakufungwa CCTV Camera 306 kuzunguka ukuta wa Mirerani wilayani Simanjro Mkoani Manyara nakukabidhiwa kwa jeshi,bilionea wa Kitanzania Saniniu Laizer ambaye amepata madini ya Tanzanite yenye thamani tofauti tofauti amezungumza nakusema kwamba awali walikuwa wanaishi kwa wasiwasi kutokana na kukosekana kwa ukuta pamoja na camera

Bilionea Laizer amepata madini ya tanzanite kwa nyakati tofauti ikiwemo aliloliuzia serikali kwa shilingi  billioni 7.8 pamoja na lingine lenye  kilo 6.3 aliloliuza  kwa shilingi  bilioni 4.8.

VIDEO ZIKIONYESHA JINSI CAMERA 306 ZINAVYOFANYA KAZI KWENYE UKUTA WA MIRERANI

Chanzo: Millard Ayo