0

Balozi Uswis: Kipaumbe changu ni madini na usindikaji wa chakula.

Mon, 5 Oct 2020 Source: habarileo.co.tz

Balozi wa Uswizi hapa nchini Didier Chassot amebainisha kuwa vipaumbele vyake vya kwanza kama balozi wa nchi hiyo ataviweka katika upatikanaji wa ajira ili kuongeza kipato binafsi, afya na kujenga mazingira ya kibiashara baina ya nchi hizi mbili, hasa katika sekta ya madini na usindikaji wa chakula.

amesema pia atahakikisha anafanya ushawishi wa kutosha kwa makampuni ya nchi hiyo kuja kuwekeza hapa nchini.

Balozi Didier amesema hayo mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho kwa Rais John Magufuli, muda mchache uliopita Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema uhusiano wa Tanzania na Uswizi ni wa muda mrefu ndio maana kuna makampuni mbalimbali ya nchi hiyo hapa nchini,

Chanzo: habarileo.co.tz