0

Wilder amfukuza kazi mkufunzi wake, kisa taulo

Wed, 26 Feb 2020 Source: mwananchi.co.tz

Bondia Deontay Wilder amemfukuza kazi mkufunzi wake Mark Breland akikasirishwa na kitendo cha mkufunzi huyo kurusha taulo ulingoni na kumpa ushindi Tyson Fury. Wilder amesema bado kulikuwa na raundi tano za pambano hilo na alikuwa na uwezo wa kumaliza na kumshinda mpinzani wake huyo. Mkufunzi huyo wa Wilder ilitupa taulo katika raundi ya saba ya pambano hilo ili kumuokoa bondia huyo aliyekuwa akivuja damu mdomoni na sikioni, pia akiwa ameangushwa mara mbili awali. Baada ya pambano hilo Wilder na mkufunzi mkuu wa timu hiyo, Jay Deas walionyesha kutokubaliana na kitendo cha mwenzao kurusha taulo ulingoni.

Chanzo: mwananchi.co.tz