0

Timaya atamba kufanya vizuri

Mon, 23 Nov 2020 Source: habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI kutoka Nigeria, Inetimi Timaya Odon 'Timaya' ameachia rasmi albumu yake mpya ya 'Gratitude' anayodai itatoa changamoto kwa wasanii wenzake.

Timaya mwenye umri wa miaka 40 alianza rasmi sanaa ya muziki mwaka 2005 na ngoma yake ya kwanza ilikuwa ‘Dema Mama’ na aliendelea kutoa kazi mfululizo na kuachia albumu yake ya kwanza ambayo aliipa jina la ‘True story’.

Baadaye aliachia album kama Gift and Grace, De rebirth, Epiphany, Linp, Upgrade na zingine nyingi na tayari ameshafanya kazi na wasanii wengi kama Patoranking, Burnaboy, Sean Paul, Phyno, Ali Kiba na wengine wengi.

Akiwa anatimiza miaka 15 toka ameanza kazi ya muziki hatimaye Timaya ameamua kutoa zawadi ya album kwa mashabiki zake ambayo ameipa jina la "Gratitude"aliyoachia wiki hiii.

"Ni sehemu ya kushukuru kwa Mungu pamoja na mashabiki wangu kwa mafanikio ambayo nimeyapata tangu nimeanza rasmi sanaa ya muziki mpaka leo,"alisema.

Album hiyo ya 'Gratitude imesheheni nyimbo kali zenye ujumbe mkubwa kama vile Gragra, I can't kill myself, The mood, Born to win, No limit, The light na zingine nyingi.

Pia tayari Ameachia video ya ngoma ya 'Gragra' kutoka kwenye album hiyo na mapokezi yake yamekuwa makubwa kwenye mtandao wa Youtube.

Chanzo: habarileo.co.tz