0

TikTok yaitetemesha Facebook, Instagram

Mon, 9 Mar 2020 Source: mwananchi.co.tz

Programu inayokuja juu ya TikTok imeanza kuzitishia programu kongwe kama Facebook na Instagram.

Tovuti mbalimbali za utafiti wa data ikiwamo Sensor zimebainisha kuwa programu hiyo imeshapakuliwa na zaidi ya watu bilioni 1.5 kwenye soko la programu za simu Google play na Play store.

Programu hiyo ilishika nafasi ya tatu nyuma ya WhatsApp na Messenger, hivyo kwa mwaka jana ilipakuliwa zaidi na kuzizidi Facebook na Instagram ambazo zilishika nafsi ya nne na ya tano. Huku ikiipita Instagram kwa kupakuliwa kwa zaidi ya watu milioni 238. Wakati Facebook wakijitahidi kuvutia watumiaji vijana wa kizazi cha kati, TikTok nao unakuzwa na watumiaji wa rika hilo.

TikTok inawavutia vijana wengi kwa sababu ya uwepo wa video za vichekesho zinazoweza kutengenezwa na mtumiaji, wepesi wa kuhariri video na kuongeza manjonjo upendavyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz