0

Tanasha: Diamond Platnumz Hatoi Matumizi ya Mtoto Wetu

Fri, 5 Jun 2020 Source: TanzaniaWeb

Tanasha Donna, ambaye anatamba na wimbo aliotoa hivi karibuni ulipokelewa vyema na mashabiki uitwao ‘sawa’, amesema kuwa baba wa mwanaye Diamond Platnumz hatoi matumizi ya kifedha kwa ajili ya mtoto wao, Naseeb Junior.

Katika mahojiano na mtangazaji Felix Odiwour, maarufu kama Jalango, Tanasha alisema kuwa anamhudumia mwanaye huyo na wala hahitaji msaada wa Diamond Platnumz.

’Nikiwa mkweli, nimekuwa nikimhudumia mwenyewe, nasema ukweli kwa asilimia 100. Mimi ni mkweli na sintosema kitu ambacho si cha kweli, pamoja na kwamba ninamuheshimu (Diamond) na sina chuki nae. Hatoi huduma kwa mwanaye na ninafanya yote mwenyewe na niseme ukweli wala sihitaji msaada wake. Ninamlea mwanangu vizuri tu, hakuna ambacho anakikosa katika maisha yake. Yupo vizuri’’, alisema Tanasha.

Hazijapita siku nyingi tangu Tanasha aliposema kuwa kwasasa yeye na Diamond wapo vizuri na wanashirikiana kulea mtoto wao ili kuhakikisha kuwa Naseeb Junior anapata upendo wa kutosha kutoka kwa wazazi.

Akiulizwa kuhusu yeye kuacha kuwafuata Diamond na memba wengine wa WCB mtandaoni, Tanasha amesema kuwa aliamua kufanya hivyo ili kuepuka kumbukumbu za kila mara kuhusu kuvunjika kwa penzi lao.

‘’Unajua nilipoachana na Diamond, mimi nipo na udhaifu wa kukasirika wakati mwingine, ni moja kati ya udhaifu wangu. Niliona kama kwakuwa kwasasa nipo Instagram, na ndiyo namna inayonisaidia kupata kipato, kwakuwa natumia muda mwingi mitandaoni kwaajili ya kazi zangu na ninawafuata hawa watu nitakuwa kwenye kumbukumbu za mambo niliyokuwa napitia.

Anaongeza kwa kusema kuwa ‘’hivi sasa, nimepona maumivu yang una mimi na baba mtoto tupo vizuri, tunaongea. Sisi si maadui, tunawasiliana kwaajili ya mtoto wetu na ninamuheshimu yeye na kila mmoja anayefanya nae kazi lakini nipo katika wakati ambao, unajua kwakuwa unapitia kuvunjika kwa uhusiano, basi kuna maumivu na nilihisi kwamba kwa kuacha kuwafuata mitandaoni kutasaidia kupunguza maumivu, Nikawa-unfollow ili nisione kile kinachoendelea’’ anasema Tanasha

Chanzo: TanzaniaWeb