0

P Diddy aibariki albamu ya Burna Boy

P Diddy aibariki albamu ya Burna Boy

Sat, 8 Aug 2020 Source: MTanzania

LAGOS, NIGERIA

BAADA ya kufanya vyema kwa albamu, The African Giant, staa wa muziki nchini Nigeria, Burna Boy, ameweka wazi ujio wa albamu nyingine, Twice As Tall ikiwa imesimamiwa na mkongwe wa Hip hop Marekani, P Diddy.

Burna Boy, ameliambia The New York Times kuwa albamu hiyo itatoka Agosti 14, mwaka huu ambapo P Diddy amehusika kama mtayarishaji mkuu (Executive Producer).

Aidha, Burna Boy alisema albamu hiyo aliiandaa katika kipindi cha corona kwa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Diddy ambaye pia ameshiriki kutoa sauti katika baadhi ya nyimbo.

Chanzo: MTanzania