0

Olenga awashukuru mashabiki kwa sapoti

Tue, 30 Jun 2020 Source: TanzaniaWeb

KUTOKA Chicago, Illinois nchini Marekani, mwimbaji wa Injili, Okito Olenga, amewashukuru wapenzi wa muziki huo kuipokea video ya wimbo wake ‘Kuna’ uliotoka hivi karibuni.

Okito mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ameliambia MTANZANIA jana, anashukuru mapokezi yamekuwa mazuri huku mashabiki wengi wakionyesha kubarikiwa na wimbo huo.

“Naamini kwenye msalaba matatizo na shida zingine za Dunia zimekwisha ndio maana nimeamua kuja na ujumbe wa namna hii ili watu wengi wabarikiwe na wajifunze kumtegemea Mungu, video ya Kuna tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube kila mmoja anaweza kwenda kuitazama,” alisema mwimbaji huyo.

Chanzo: TanzaniaWeb