0

Nyimbo zampa Tanasha kigugumizi

Wed, 20 Jan 2021 Source: habarileo.co.tz

MSANII, Tanasha Donna amesema ana wakati mgumu wa kuchagua wimbo wa kuanza kuachia kwa mwaka huu kutokana na kuwa na nyimbo nyingi kwenye maktaba yake.

Msanii huyo amesema nyimbo hizo ni za aina mbalimbali kitu ambacho kinamchanganya zaidi kujua upi uanze kutoka kwa ajili ya mashabiki wake.

“Nina nyimbo nyingi katika maktaba yangu na nyingine nilizoshirikisha wasanii wengine hivyo, napata wakati mgumu kuchagua nianze kutoa upi,” ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Februari mwaka jana Tanasha aliachia ‘EP’ yake ya kwanza tangu kuanza muziki iliyoitwa DonnaTella.

EP hiyo ilikuwa na ngoma nne ambazo ni ‘Vie’ aliomshirikisha Mbosso, pia kuna ‘Gere’ ambao ameshirikisha Diamond Platnumz, kuna ‘Ride’ aliomshirikisha rapa Khaligraph Jones na ya mwisho inaitwa ‘Te amo.’

Chanzo: habarileo.co.tz