0

Ndiyo Huyu Sasa: Picha Kali ya Lupita Nyong'o na Bae Wake

Sat, 27 Mar 2021 Source: kiswahili.tuko.co.ke

- Lupita alionekana kwenye picha hiyo na ndume aliyesema huiyeyusha roho yake pakubwa

- Baadhi ya wanamtandao walipekua picha hiyo zaidi na kuona huenda akawa anatarajia baraka zaidi

- Lupita alipata umaarufu baada ya kuigiza katika filamu ya 12 Years a Trade

Muigizaji Lupita Nyong'o hatimaye amefungua roho kuhusu jamaa anayempenda na kumtumia ujumbe mtamukupitia mtandao.

Lupita, ambaye sifa yake ya uigizaji imemfanya kutamba dunia nzima, alisema huyo ndiye ndume ambaye humsisimua.

Aliyasema hayo kwenye picha tamu aliyoipakia katika ukurasa wake wa Facebook akimtambulisha ndume huyo kwa ulimwengu.

Alisema walikutana miaka 24 iliyopita na alipomuona aliishiwa na nguvu kwenye magoti yake na ndipo akajua amempata wake."Nilikutana na Saheem Ali miaka 24 iliyopita na kila mwaka hujipata naendelea kumpenda zaidi," aliandika mtoto huyo wa Kisumu.

Alisema ombi lake nipenzi lao kuendelea kushika mizizi sawa na talanta zao kwani ndume huyo pia yuko kwenye usanii wa uigizaji.

Kulingana na ujumbe wa Lupita, Saheem pia huwa ni mwelekezi wake na kwa sasa anafanya hivyo katika moja wapo wa vipindi anavyoigiza.

Muigizaji huyo alisema Saheem amekuwa ulimwengu wake na kila wakati wanajipata pamoja hufurahia kifua chake.

"Yeye ni mwandani wangu, ndume anayenipautulivu moyoni na rafiki wa kujivinjari naye kwenye ziara za likizo. Pia yeye hunilinda," alisema Lupita.

Kutokana na ujumbe wa kipusa huyo, ni wazi kuwa ndume Saheem ameupenya moyo wake inavyostahili.Lupita ni mwanawe mwanasiasa mkongwe Profesa Anyang' Nyong'o ambaye kwa sasa ni gavana wa Kisumu.

Alipata umaarufu mkubwa baada ya kucheza uigizaji katika filamu za Shuga na pia '12 Years a Slave'.

Ni binti mwenye talanta ya juu na amekuwa akitamba katika sekta ya filamu Marekani ambapo anashiriki filamu kadhaa na hata kushinda tuzo mbali mbali.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke