0

Namna ya kupunguza maombi ya urafiki Facebook

Mon, 17 Feb 2020 Source: mwananchi.co.tz

Mtandao wa kijamii wa Facebook umekuwa chanzo cha watu kujuana.

Mtu akijiunga anatuma maombi kwa watu anaokutana nao huko na kisha wanajuana na watu kutokana na kutumiana maombi ya urafiki na ukakubali, pengine tangu umejiunga Facebook una marafiki zaidi ya 500.

Japokuwa kuna wengine wamesharidhika na idadi ya marafiki walionao lakini bado wanapokea maombi ya urafiki kutoka kwa watu mbalimbali, wengine huachana na hayo maombi.

Fahamu kuwa kuna njia ya kuondokana na usumbufu huo kwa kuingia kwenye Settings kisha nenda kwenye Privacy.

Kisha chagua kipengele cha Friends of Friends ambacho sasa kitakuwezesha kupokea ombi la urafiki iwapo tu anayekuomba urafiki ni rafiki wa rafiki yako.

Chanzo: mwananchi.co.tz