0

Mzimbabwe anaetamba kwenye midundo ya wasouth (Amapiano)

Sat, 19 Dec 2020 Source: millardayo.com

NI  mrembo mwenye  umri wa miaka 26 mzaliwa wa Zimbabwe ambae kwasasa ndie anatikisa muziki wa Afrika kusini uitwao Amapiano, Mrembo huyo amejipatika umaarufu baada ya kusikika kwenye rekodi kadhaa zilizotayarishwa na wakali waitwao Scorpion Kings (Dj Maphorisa & Kabza De Small).

Sha Sha mpaka sasa ameshafanya rekodi kadhaa tu ikiwemo Tender Love, Sing it Back, Woza ndizo ambazo zimempa umaarufu hususani kupitia muziki unaotambulika kwa jina la Amapiano.

Mbali na kwamba hivi karibu aliweza kushinda tuzo ya Best New International Act sasa time ametuletea video mpya ya wimbo wake uitwao Woza unaweza kuitazama hapa

Chanzo: millardayo.com