0

Mwanamuziki wa nyimbo za Benga Albert Gacheru ameaga dunia

Tue, 6 Apr 2021 Source: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za aina ya Benga Albert Gacheru Wamaitu ameaga dunia akipokea matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta.

Wamaitu aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 59 na alivuma kwa kibao chake maarufu Mwendwa Wakwa Mariru miaka ya tisini.

Vibao vingine alivyovuma navyo ni Mumunya,Hurry Hurry Waithera Nindaguteire na Indo Ciakwa.

Nyimbo zake zilipendwa na jamii kadhaa na hata zilikuwa zikichezwa kwenye stesheni za kimataifa ikiwemo Voice of America.

TUKO.co.ke imefahamishwa kwamba marehemu ameugua kwa muda mrefu.

Mashabiki wake mitandao pamoja na wasanii wenzake wameomboleza kifo chake.

" Nimepokea habari za kifo cha mwanamuziki Albert Gacheru Wamaitu kwa mshtuko,nilikuwa namtazamia sana niliokuwa mwanamuziki chipuka, tutamkosa sana," Jaguar aliandika.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke