0

Mtoto wa JAY Z na tuzo ya BET

Tue, 30 Jun 2020 Source: TanzaniaWeb

MTOTO wa rapa Jay Z, Blue Ivy Carter, amekuwa mmoja kati ya wale waliochukua tuzo za BET nchini Marekani usiku wa kuamkia juzi.

Blue Ivy Carter mwenye umri wa miaka nane, ameanza kufuata nyayo za wazazi wake Jay Z na Beyonce, baada ya kuchukua tuzo hilo ikiwa ni msanii aliyeshirikishwa kwenye wimbo wa mama yake ambao unajulikana kwa jina la Brown Skin Girl.

Wimbo huo wa Beyonce umewashirikisha wasanii wengine kama vile WizKid na SAINt JHN, hivyo wasanii wote walioshiriki kwenye wimbo huo wanahusika kwenye tuzo hiyo.

Hii sio tuzo ya kwanza kwa wimbo huo, tangu umeachiwa umefanikiwa kuchukua tuzo zingine kama vile 2019 BET Soul Train na 2020 NAACP Image Awards.

Chanzo: TanzaniaWeb