0

Mtayarishi wa kipindi cha The beat Arthur K afiwa na babake

824c3b9954cce8da Mtayarishi wa kipindi cha The beat Arthur K afiwa na babake

Thu, 8 Apr 2021 Source: kiswahili.tuko.co.ke

Mtayarishi wa kipindi cha The Beat Arthur K anaomboleza kufuatia kifo cha babake mzazi kilichotokea Alhamisi, Aprili 8

Arthur alitangaza habari za kifo cha babake kuptia mtandao wa kijamii wa Instagram huku akielekezea jinsi atakavyomkosa.

Kwa wale wanaopenda kutizama vipindi vya muziki ,basi jina Arthur K sio geni kwani ndiye mtayarishaji wa kipindi cha "The beat" ambacho hupeperushwa kwenye runinga ya NTV.

Jarida la TUKO.co.ke limefahamishwa kwamba Arthur K na familia yake wanaomboleza kifo cha mpendwa wao ila tu haijabainika alikuwa akiugua ugonjwa upi.

Akimuomboleza babake, Arthur K amemtaja kama mtu mtulivu na mwenye amani na Mcha Mungu.

"Babangu, mtu niliyemtegemea sana, Mcha Mungu na kiongozi katika jamii, alikuwa mtulivu, mpenda amani na msema ukweli. Kasisi Ngeru ameaga dunia na kwa sasa hatutakuwa pamoja tena,

Hata hivyo najua uko mahali Pema. Ulinipea chochote nikichotaka. Pumzika vyema babangu. Waefeso 4:11-13." Arthur aliweka Instagram.

Mashabiki wa Arthur wameomboleza kifo cha babake kwa kumtumia salamu za pole.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke