0

Mtayarishaji movie aliyoigiza Wema, Van Vicker atwaa tuzo Marekani

Thu, 17 Dec 2020 Source: millardayo.com

Cop’s Enemy moja kati ya filamu zilizofanya vyema zaidi kwa mwaka 2020 imeweka rekodi baada ya kufikisha watazamaji zaidi ya Million 1 kwa kipindi cha miezi minne tu.

Licha ya mafanikio hayo John K-ay ambaye ndio mtayarishaji wa filamu hiyo pia amefanikiwa kuchukua tuzo nchini Marekani “The African Film Festival in Dallas” kupitia filamu ya Cop’s Enemy na kufanikiwa kushinda katika kipengele cha Mtayarishaji filamu anayechipukia.

Katika tuzo hizo alikua akishindanishwa na wakali wa filamu kutoka nchi mbalimbali Africa.

Ikumbukwe Cop’s Enemy imewashirikisha wasanii wakubwa kutoka Africa na nje ya Africa kama John k-ay, Van Vicker pamoja na Wema Sepetu na imeongozwa na Neema Ndepanya kutoka Tanzania pamoja na Prema Smith toka Australia.

MILIMA NA MABONDE, MAISHA YA MATUKIO “NIMEFANYA KAMPUNI YA R.KELLY, NIMEMPOTEZA BABA, MAMA”

Chanzo: millardayo.com