0

Msanii wa Nigeria avutiwa na mazingira ya Tanzania

Mon, 21 Dec 2020 Source: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki kutoka Nigeria, Enoch Solomon ‘NiftyBoi’ amesema Tanzania kuna madhari nzuri ndio maana amekuja kufanya video ya wimbo wake uitwao Different Vibe.

Akizungumza Dar es Salaam juzi alisema amevutiwa na mandhari ya Tanzania hasa Dar es Salaam ndiyo maana amechagua kuja kufanya video yake hapa.

“Tanzania kuna mazingira mazuri ambayo yanapendeza katika video ndio sababu iliyonifanya nije kufanya kazi yangu pia hapa tasnia ya muziki inakua kwa kasi,” alisema Nifty Boi.

Aliongeza kuwa mbali na mazingira ya Tanzania ni nchi ya amani na watu wake ni wakarimu hivyo ni rahisi katika kufanya kazi.

Mbali na Nifty Boi kuja kufanya video hapa nchini hivi karibuni msanii mkongwe wa dansi Koffe Olomide naye alikuja Tanzania kwa ajili ya kurekodi video ya nyimbo yake ambayo aliahidi kuitoa siku za usoni.

Chanzo: habarileo.co.tz