0

Msanii Stivo Simple Boy aloweshwa na mapenzi ya kidosho Mzungu

Tue, 13 Apr 2021 Source: kiswahili.tuko.co.ke

- Stivo Simple Boy ameibua zogo mitandaoni baada ya kuchapisha picha akiwa ametulia na mrembo wa Kizungu

-Wakenya walijitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu picha hiyo

- Mwimbaji huyo aliwahi kutangaza ni bikra

Stivo Simple Boy ameibua zogo mitandaoni baada ya kuchapisha picha akiwa ametulia na mrembo wa Kizungu.

Kwenye picha hiyo ya Jumatatu, Aprili 12, msanii huyo anaonyeshwa akiwa ametulia na mrembo kifuani ambapo huenda alikuwa usingizini.

Alitumia ujumbe wa kitambulisho chake "ndio maanake"pamoja na emoji za mapenzi kuchapisha picha hiyo, na kuchangamsha mtandao.

Huku baadhi ya wafuasi wake wakimpongeza mwimbaji huyo wa Mapenzi Ya Pesa kwa kumtambulisha mrembo huyo, wengine walimuomba kuwa jasiri.

@irrizwarririz: "Heri nyinyi."

@jbjokes_kenya said: "Hii ni fire."

@mukami___ki: "Stivo acha uoga."

@mcjacci: "Kumekucha."

@bigg_muller: "Rada smart sana."

"Stevo yaaani uko na mzungu," @bertdah alisema.

@skillah_169: "Huyu mzungu pia anataka pesa."

NdoaHuku akidai bado ni bikra, Stivo katika mahojiano ya awali alisema wanawake wengi wanamuomba pete ya uchumba lakini alisema bado anataka kusubiri.

"Warembo huniambia Ah Simple Boy nakupenda na ninataka kukuoa. Lakini mimi huwambia kusubiri hadi Mungu atakapoamua kisha nitaoa," alisema katika mahojiano na mwanahabari wa TUKO.co.ke, Lynn Ngugi.

Akiulizwa mbona hajapata mchumba Stivo alisema kumpata mke mwema ni kibarua kigumu na kuwaomba warembo wampe muda.

Stivo pia alitaja aina ya mwanamke ambaye angelipenda kumuoa akisema anatakiwa kuwa ameokoka.

"Naangalia tabia, anatakiwa kuwa mwaminifu kwangu, kisha heshima na kuokoka," aliongezea.

Dhuluma mtandaoniStivo amekuwa akidhulumiwa mitandaoni kutokana na muonekano wake huku sura yake ikitumika kwenye memes za ucheshi lakini amejifunza kupuuza.

TUKO.co.ke iliripotia kuwa meme iliyokuwa na sura yake ilimvutia rapa maarufu wa Marekani Snoop Dogg.

Katika picha hiyo, kichwa cha Stivo kilikuwa kimebandikwa kwenye mwili wa mwanamke.

Baadhi ya Wakenya hawakufurahishwa na posti ya Snoop huku wakimshtumu vikali.

Lakini Stivo alichapisha picha hiyo na hata kumshirikisha Snoop.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke