0

Master KG kufanya kolabo na Harmonize

Mon, 14 Dec 2020 Source: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki kutoka Afrika aliyetamba na wimbo wake wa ‘Jerusalema ‘, Master KG amewaambia mashabiki wa Harmonize kuwa watarajie kolaba na yeye.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Master KG alisema Harmonize amekuwa rafiki wake hivyo mashabiki wategemee jambo lolote kutoka kwao.

“Mashabiki wa Harmonize watarajie kolabo ya mimi na yeye maana tumekuwa marafiki wakubwa,” alisema Master KG.

Master KG amekuwa maarufu zaidi duniani kupitia wimbo wake wa Jerusalema ambao video yake imeweza kutazamwa zaidi ya mara milioni 200 kwenye mtandao wa YouTube ndani ya mwaka mmoja.

Msanii huyo yupo nchini ambapo jana alitarajiwa kufanya onesho Golden Tulip Oysterbay, Dar es Salaam.

Chanzo: habarileo.co.tz