0

Mapokeo ya "Back To Back" yamshangaza Remiray

Tue, 30 Mar 2021 Source: mtanzania.co.tz

Msanii wa kizazi kipya mwenye makazi yake nchini Canada, Remiray Music, ameshangazwa na mapokezi makubwa ya wimbo wake, Back To Back aliomshirikisha staa wa Cameroon, Peti Pays.

Remiray, amesema wimbo huo unafanya vizuri kwenye mitandao yote ya kusikiliza na kupakua muziki (music platforms) tofauti na matarajio yake.

“Wimbo ulirekodiwa miaka mitatu iliyopita ambapo Peti Pays alikuja huku Toronto na sasa tumeona muda mwafaka wa kuachia Back To Back, wimbo tayari unapatikana kwenye majukwaa yote, hivyo nahitaji uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki zangu wa Afrika,” amesema Remiray.

Chanzo: mtanzania.co.tz