0

Lovy Logomba Atua Kenya Baada ya Kifo cha Kakake, Akutana na Nameless, Wahu

Wed, 31 Mar 2021 Source: kiswahili.tuko.co.ke

- Wanamziki Nameless na mkewe Wahu walijawa na furaha baada ya kukutana na Lovy Longomba ambaye mara ya mwisho kuonana ilikuwa miongo miwili iliyopita

- Kulingana na picha walizo pachika mtandaoni, wawili hao walionyesha furaha isiyo na kifani kupatana na rafiki yao wa zamani

- Lovy na nduguye marehemu Christian waliondoka nchini kwenfa Marekani kutafuta riziki zaidi baada ya kuvuma katika ulingo wa muziki hapa Kenya

Mwanamuziki Lovy amerejea nchini kujumuika na marafiki pamoja na jamaa zake, baada ya kuishi Marekani kwa zaidi ya miongongo miwili.

Lovy ambaye kwa sasa ameokoka na anajiita nabii, alikutana na wasanii Nameless na mkewe Wahu ambapo walikuwa na wakati mzuri.

Mwanamuziki Nameless hakuficha furaha yake aliposti picha ya watatu hao mtandaoni huku akisifia uhusiano wao licha ya kutoonana kwa muda mrefu.

Nabii Lovy aliwasili nchini March 26, na kupokelewa vema na marafiki aliowaacha hapa Kenya miaka mingi iliyopita.

Aidha, kabla ya kurejea kwa Lovy alikua amechapisha mitandaoni kwamba angerejea nchini Jambo ambalo wafwasi wake hawakutilia maanani.

"Najihisi vyema kurudi nyumbani, nafurahia kabisa kuwa nyumbani," Alisema Lovy

Kwa sasa Lovy Longomba anakutana na jamaa na marafiki kuwafahamisha kuhusu kifo cha nduguye Christian ambaye aliaga hivi majuzi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke