0

Kusomwa kwa Bajeti: Barabara za jiji zafungwa ili waheshimiwa wapite

Thu, 10 Jun 2021 Source: kiswahili.tuko.co.ke

Serikali imetangaza kufungwa kwa barabara kadhaa za jiji leo ili kuruhusu waheshimiwa waweze kuhudhuria kikao cha kusomwa kwa bajeti.

Kulingana na mshirikishi wa Nairobi James Kianda, Wizara ya Usalama wa Ndani itachukua hatua hiyo ili kuzuia msongamano.

Barabara za Parliament, Harambee Avenue, Taifa Road na City Hall Way zitafungwa leo kati ya saa saba mchana na kumi na moja jioni.

"Zitafungwa kati ya saa saba mchana na saa 5:30 p.m leo ili kuwapa wabunge, maseneta na maafisa kutoka Hazina ya Kitaifa muda wa kufika bungeni," Kianda alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke