0

Kumbe Bieber anahusika urembo wa mke wake

Wed, 20 May 2020 Source: TanzaniaWeb

KUPENDEZA kwa mwanamitindo Hailey Bieber ambaye ni mke wa staa wa muziki wa pop nchini Marekani, Justin Bieber kunatokana na msanii huyo.

Wawili hao wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii na kuposti picha ambazo zinamuonesha Bieber akimfanyia urembo mke wake huyo.

“Kupendeza kwa mke wangu kunatokana na mimi mwenyewe hasa kwa kipindi hiki cha virusi vya corona kwa kuwa hakuna muda wa kwenda saluni, kazi zote ninazifanya mimi na anazidi kuonekana kuwa mrembo duniani,” aliandika Bieber.

Wawili hao wamekuwa wakikaa ndani kwa muda mrefu kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya corona ambavyo vinatikisa dunia.

Chanzo: TanzaniaWeb