0

Koffi asema dansa aliyempiga Kenya bado yupo naye

Thu, 12 Mar 2020 Source: mwananchi.co.tz

Mwanamuziki wa DRC Kongo, Koffi Olomide, amesema mcheza shoo wake ambaye alimpiga na kusababisha kufukuzwa Kenya bado yupo naye.

Koffi ameyasema hayo jana Machi 10, 2020 katika  mkutano wake na waandishi wa habari nchini Kenya ambapo yupo huko kwa ziara ya kimuziki.

Julai mwaka 2016 mwanamuziki huyo alijikuta akiingia matatani na vyombo vya dola baada ya akimpiga mateke mmoja wa madansa wake wakiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata, ambapo walikuwa wanaenda kwa ajili ya kufanya shoo.

Kitendo hicho kiliibua gumzo mitandaoni na kusababisha kutolewa kwa matamko mbalimbali kutoka kwa wanaharakiti wanaotetea haki za wanawake jambo lililopelekea kufutwa kwa onyesho lake na kufukuzwa.

Ikiwa imepita miaka mine sasa, juzi msanii huyo alikwenda Kenbya akiwa anatokea Tanzania na jana alizungumza na wanaadishi wa habari masuala mambalimbali na moja ya mambo ambayo waandishi walimuuliza ni kuhusiana na kitendo alichofanya cha kumpiga dansa huyo.

Kokatika majibuyake , amesema huwa hapendi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa sio kitendo cha kujivunia na kukiri kwamba kilikuwa ni kitendo cha aibu kwake na bendi yake ya ..huku akikiri aliwakosea wanawake hususani wa Kenya na ndio maana hajawahi kuongea lolote tangu kutokea kwa tukio hilo.

Pia Soma

Advertisement
Pia alimlaumu mpiga picha aliyechukua video hiyo ambaye ameeleza walifanya naye mahojiano ya takribani dakika kumi baada ya kutokea kwa tukio kueleza sababu ya kwa nini alifikia hatua ya kumpiga dansa huyo lakini hakuwahi kurusha.

“Mimi ni binadamu nakiri kitendo nilichofanya kwa dansa wangu hakikuwa kizuri, nitumie nafasi hii kuwaomba wanawake msamaha na wajue kwamba nawapenda sana na ipo siku nitakuja kufanya show  kwa ajili yao.

“Pia nataka watambue kwamba hata yule dansa niliyempiga msanii hadi leo bado nipo naye kwani mimi ni mkiristo nimefundishwa kusamehe hivyo niliamua kumsamehe na kuacha maisha yaendelee,”amesema mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa anatesa na wimbo wa Papa Ngwasuma.

Hata hivyo amesema hii ni mara yake ya 27 kwenda nchini Kenya na hajawahi kufanya jambo lolote baya nchini humo, hivyo siku hiyo ilitokea tu..

Chanzo: mwananchi.co.tz