0

K-6 kufanya makubwa Julai

Thu, 25 Jun 2020 Source: TanzaniaWeb

BAADA ya kufanya vizuri na albamu yake fupi (EP) ya Carry Me Go, mwanamuziki mwenye asili ya Gambia anayeishi Utah, Marekani, Sulayman Sarr a.k.a K-6, amejipanga kuwapa raha zaidi mashabiki mapema Julai, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, K6, alisema licha ya kuwa anaishi Marekani anaamini katika mashabiki waliopo Afrika ndio maana muziki wake huwa una vionjo vingi vya kiafrika.

“Nashukuru EP yangu ya Carry Me Go ambayo nilishirikiana na BO, imefanya vizuri sana, sasa natarajia Julai 1, mwaka huu nitaachia ngoma yangu mpya ambayo itapatikana kwenye mitandao mbalimbali kama vile Spotify, Amazon, YouTube na mingine mingi kikubwa ni sapoti,” alisema K-6.

Chanzo: TanzaniaWeb