0

Jose Chameleone atua Tanzania kumuaga Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Source: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Uganda, Jose Chameleone ametua nchini Tanzania kwa ajili ya kuungana na Watanzania katika ibada ya kumuaga Rais John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Leo Jumatatu Machi 22, 2021 ibada ya kutaifa ya kumuaga kiongozi huyo inafanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dodoma.

Mwanamuziki huyo aliwasili nchini jana akiwa na mwenzake Pallaso Music.

Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram ameweka video fupi inayoeleza ujio wake na kuandika, “Ndugu zangu wabongo poleni sana kwa msiba mkubwa wa Rais mpenda wanyonge. Hili ni pigo kubwa ila Mungu atawavusha. Weekend mimi na ndugu wangu Pallaso music tunawakilisha Uganda tunaungana  nanyi kumuaga Rais Magufuli. Mungu ametoa Mungu ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz