0

Inasikitisha mrembo Moana alijitabiria kifo, afariki kwenye ajali na Bilionea Ginimbi

Inasikitisha mrembo Moana alijitabiria kifo, afariki kwenye ajali na Bilionea Ginimbi

Wed, 11 Nov 2020 Source: Millard Ayo

NI Headlines  za Genius Kadungure aka Ginimbi ambae usiku wa kuamkia Novemba 8 Jumapili alifariki Dunia akiwemo na marafiki zake watatu ambao ni Michelle Amuli a.k.a Moana, Limumba Karim wa (Malawi) pamoja na Elisha (Raia wa Msumbiji) katika ajali ya gari aina ya Rolls Royce iliyogonga magari matatu kisha kuelekea kwenye mti na kuwaka moto huko nchini Zimbambwe.K

Kwasasa kinachoendelea mitandaoni ni kuhusu Mrembo Moana ambae mwaka 2019 Mwezi May aliwahi kujikoredi video huku akielezea namna anavyopitia wakati mgumu kwa kile kinachomnyia kwenye ndoto na huku akidai anahisi kama atakuwa kwenye giza zito kisha  atashindwa kupumua  huku akihitaji msaada lakini hatofanikiwa kuupata msaada wowote na ndio utakuwa mwisho wake.

Sasa hicho alichokisema Moana yaani ni kama alijitabiria Kifo kwani kwenye ile Ajali ya Gari aliyokuwemo ya Bilionea Ginimbi ambayo iligonga Magari matatu kisha kugonga mti na kulipuka zilisikika sauti za warembo wawili ambae ni Moana na Elisha zikihitaji  msaada lakini mwisho wa siku hawakufanikiwa kupata msaada na umauti ukawakuta. kwahiyo huenda alijitabiria kifo lakini hakujua nini kitakachomjia mbeleni.Pumzika kwa Amani Moana & Elisha, Ginimbi & Karim.

ITAZAME HII VIDEO HAPA UJIONEE VIDEO YA MOANA INAYOHISIWA KUWA ALIJITABIRIA KIFO

JIPYA LAIBUKA! SIMANZI YAONGEZEKA MAZISHI YA MOANA, MAMA YAKE ASEMA HAWATAMZIKA MPAKA HILI LIFANYIKE

Chanzo: Millard Ayo