0

Forbes waitaja Serengeti kama kivutio cha lazima kutembelea 2021

Safaro Tours To Serengeti National Park 1200x675 1 660x400 Forbes waitaja Serengeti kama kivutio cha lazima kutembelea 2021

Fri, 20 Nov 2020 Source: Millard Ayo

Jarida la Forbes la nchini Marekani, limeitaja Serengeti kuwa kivutio cha pili kuvutia kutembelewa na watalii zaidi kwa mwaka 2021.

Serengeti imetajwa kuwa na uhamiaji mkubwa zaidi wa wanyama duniani “largest terrestrial mammal migration in the world,” ambayo imeifanya Serengeti kuwa moja kati ya maajabu saba ya Asili Afrika.

Pia, ni sehemu ambayo mtalii anabahatika kuona aina mbalimbali za wanyama kwa kipindi kifupi.

Kivutio kilichoshika nafasi ya kwanza ni Kisiwa cha Maldives kilichopo bara la Asia. Maldives imewekwa katika orodha hiyo kutokana na kuwa na muonekano mzuri na maji yaliyo safi. Aidha, kimetajwa kuwa sehemu nzuri ya kutembelewa na wapenzi.

KINACHOENDELEA UBELGIJI BALOZI AFICHUA MAPYA, AKANUSHA UPOTOSHAJI UNAOENDELEA

Chanzo: Millard Ayo