0

Februari Ulikuwa mwezi wa mahaba, skendo na kazi

Mon, 1 Mar 2021 Source: mwanaspoti.co.tz

By Kelvin KagamboMore by this Author TUNAIMALIZIA Februari leo; mwezi ambao mandhari yake ilikuwa ni mapenzi na mahaba. Mwezi ambao kwa mujibu wa kalenda ya Gregori ndiyo mwezi mfupi zaidi ukiwa na siku 28 tu ndani ya mwaka huu. Yaani wale wote waliozaliwa Februari 29, mwaka huu hawana chao mjue!

Lakini, licha ya ufupi wake mambo kibao yametokea ndani ya mwezi huu kwenye upande wa burudani kiasi kwamba ilikuwa ni rahisi sana mfuatiliaji kupotea njiani na huenda hata wewe ulipitwa kwenye baadhi ya matukio.

Ngoma mpya zimeachiwa, albamu pia zilikuwepo, skendo, kiki na habari kubwa kubwa za burudani zilikuwa za kutosha jumlisha fujo katika Siku ya Wapendanao. Kwa kifupi, Februari ulikuwa na ujazo wa kutosha na leo tunamulikia kwa uchache matokeo yote makubwa ya burudani ya mwezi huu.

VALENTINE ILIKUWA PAMBE

Valentine ya mwaka huu ni ya kukumbukwa kwa sababu ilikuwa na sapraizi kibao kutoka kwa wasanii. Msanii wa muziki wa Bongofleva, Harmonize alichapisha kwa mara ya kwanza picha akiwa na mpenzi wake mpya muigizaji Kajala Masanja. Kabla ya kuposti picha hiyo Harmonize na Kajala walikuwa wanatajwa kuwa wanachangia kopa moja lakini mara zote walipinga.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz