0

Davido kuja na albamu mpya Julai

Wed, 6 May 2020 Source: HabariLeo

STAA wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke, maarufu kwa jina la Davido, amewataka mashabiki zake kujiandaa na ujio wa albamu yake mpya Julai mwaka huu.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 27, ameliweka wazi jina la albamu hiyo kuwa ni ‘A Better Time’ hivyo mashabiki wakae tayari kusapoti kazi hiyo.

“Julai mwaka huu nitaachia albamu mpya ambayo inajulikana kwa jina la “A Better Time.” Mashabiki kaeni tayari kusapoti kazi hiyo,” aliandika msanii huyo.

Hata hivyo, alikwenda mbali zaidi kwa kuwadokeza mashabiki hao kuwa, ndani ya albamu hiyo kuna wimbo ambao amefanya na rapa wa kutoka nchini Marekani, Nicki Minaj.

Chanzo: HabariLeo