0

Corona ‘yazuia’tuzo orona ‘yazuia’tuzo za MtvMama 2021

Mon, 8 Feb 2021 Source: habarileo.co.tz

WAANDAJI wa tuzo za muziki za Afrika, Mtv wametangaza kuahirisha hafl a ya ugawaji wa tuzo hizo za MtvMama 2021 zilizotarajiwa kufanyika Februari 20 mwaka huu Jijini Kampala Uganda kutokana na Corona.

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya MtvBase walitoa taarifa ya kuahirisha utoaji tuzo za muziki za Mtv Afrika 2021 na hawajaweka wazi zitatolewa tena lini.

Hiyo ni mara ya pili kuahirishwa kwa tuzo hizo za kimataifa zinazofanyika kila mwaka kwa sababu ya Corona.

Tuzo za MTV Mama kwa mwaka 2021 zilitarajiwa kuwakutanisha wasanii zaidi ya 30 kutoka mataifa 15 ya Afrika, huku wasanii kutoka Nigeria wakitawala kwa kutajwa mara 14 kwenye vipengele vya tuzo hizo.

Wasanii wa Tanzania waliotajwa kushiriki tuzo hizo ni Rajab Kahali ‘Harmonize’kipengele cha msanii bora wa kiume, Zuhura Soud ‘Zuchu’ (msanii anayechipukia), Rostam (kundi bora la muziki) huku Naseeb Abdul ‘Diamond’ akiingia kwenye vipengele viwili (msanii bora wa mwaka na shoo kali kipindi cha corona).

Tuzo za MTV Mama zilianzishwa mwaka 2008 maalumu kwa ajili ya wanamuziki wa Afrika na kila mwaka taifa moja kutoka Afrika hupewa kibali cha kuwa mwenyeji.

Kwa mataifa ya Afrika Mashariki ni Kenya na Uganda waliowahi kupata tiketi ya kuwa wenyeji wa tuzo hizo za kulinda na kuinua muziki wenye asili ya Afrika.

Chanzo: habarileo.co.tz