0

Chameleone ashindwa Umeya

Chameleone ashindwa Umeya

Mon, 25 Jan 2021 Source: HabariLeo

MEYA Elias Lukwago wa Chama cha FD ameweza kutetea kiti chake cha Umeya wa jiji la Kampala kwa kuwapiku wapinzani wake 10, akiwemo msanii Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’.

Msimamizi wa uchaguzi Ruwaga kitongoji cha jiji la Kampala ndiye aliyekuwa mhusika mkuu katika kuhesabu kura kwenye matokeo ya uchaguzi wa Meya wa jiji la Kampala.

”Ndugu zangu sina cha kuwaambia nina furaha kubwa watu wangu, hapa nyumbani na wakazi wote wa jiji la Kampala asanteni sana”.

Lukwago alishinda karibu kata zote tano za wilaya ya Kampala kwa mujibu wa matokeo ya mwanzo yaliotolewa katika kata zote.

Wakati huo huo, Mahakama Kuu Kampala inatarajiwa kusikiliza ombi la Robert Kyagulanyi kuachiwa huru na vikosi vya ulinzi vinavyomzuia nyumbani kwake.

Chanzo: HabariLeo