0

Cardi B amwagia sifa Nicki Minaj

Tue, 11 Aug 2020 Source: mtanzania.co.tz

LOS ANGELES, MAREKANI

RAPA machachari wa kike nchini Marekani, Cardi B, amemwagia sifa hasimu wake kwenye rap, Nicki Minaj kwa kutawala muziki katika kipindi cha miaka 10 iliyopita mfululizo.

Cardi ameueleza mtandao wa Apple Music kuwa katika makuzi yake kulikuwa na rapa wengi wa kike ila walikuja kupotea wote mpaka alipoibuka Nicki Minaj na kutawala kwa muda mrefu.

“Nikiwa na miaka sita hadi nane kulikuwa na rapa wengi wa kike ila wote walipotea, ilikuwa inanilazimu kusikiliza nyimbo za zamani, kwasababu hapakuwa na rapa wa kike lakini alitokea rapa mmoja wa kike ambaye alifanya vizuri na bado anafanya hivyo,” alisema Cardi B.

Chanzo: mtanzania.co.tz