0

Amber Rose asherehekea birthday ya mwanaye na wanaume aliozaa nao

Amber Rose asherehekea birthday ya mwanaye na wanaume aliozaa nao

Wed, 19 Feb 2020 Source: mwananchi.co.tz

Mwanamitindo maarufu nchini Marekani amesherekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake wa kwanza akiwa na wanaume wote wawili aliozaa nao.

Amber Rose  ambaye jina lake halisi ni Amber Levonchuck, ameweka picha hiyo katika ukurasa wake wa Instagram.

Katika picha hiyo ambayo Amber amevalia nguo nyeusi huku akiwa amembeba mtoto wake mdogo Slash, ilimuonyesha Alexander Edward 'AE',  akiwa ameweka mikono yake begani kwa Amber Rose na Wiz Khalifa ambaye alikuwa naye alikuwa amemkumbatia mtoto wake Bash na wote kuonekana wakiwa katika nyuso za furaha.

Mwanamitindo huyo mwenye miaka 31, ana watoto wawili ambao ni  Sebastian ‘Bash’ na Slash.

Bash ambaye jana ndio katimiza miaka saba, amezaa na aliyekuwa mume wake wa zamani Wiz Khalifa,wakati Slash amezaa na makamu wa Rais wa lebo ya muziki ya Def Jam,  Alexander Edward maarufu kwa jina la ‘AE’.

Chanzo: mwananchi.co.tz