0

#AMAPIANO: Utaipenda Mkali Kabza De Small alipokutana na Major League DJ

Sun, 17 Jan 2021 Source: millardayo.com

Najua nina watu wangu wanaofuatilia muziki wa South Africa maarufu kama Amapiano sasa time hii nimekusogezea hii burudani yenye lisaa limoja ambapo mkali Kabza De Small ameungana na wakali Major League DJ’Z kuonesha uwezo wake kwa kuzicheza nyimbo za Amapiano.

Kabza De Small ni miongoni mwa watayarishaji wanaofanya vizuri kwasasa na kama utakuwa na unakumbuka mnamo Oct 17, 2020 aliiandika historia Dar es Salaam kwa kuzicheza live nyimbo hizo maarufu kama Amapiano.

Huu ni Mwendelezo wa burudani zinazotolewa na wakali Major League DJ’Z , unaweza ukaitazama hapa video ujionee shangwe zao

Chanzo: millardayo.com