0

20 watinga fainali Miss Rwanda

Wed, 10 Mar 2021 Source: www.habarileo.co.tz

TAJI la Miss Rwanda sasa litaamliwa na warembo 20 waliovuka katika mchuano uliofanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli La Palisse huko Nyamata. Washiriki 20 wa fainali walipatikana wakati wa mchujo uliofanyika kwa njia ya video Jumamosi kwenye ukumbi wa Intare Conference Arena, Machi 6, ambao pia ulioneshwa mubashara kupitia televisheni ya RBA chaneli ya Kigali ili kuwawezesha watu kuangalia kutoka nyumbani.

Warembo hao walichaguliwa kutoka wale 37 ambao walipata ‘PASS’ kwa ajili ya kuwakilisha majimbo yao mapema katika shindano la video lililofanyika mapema wiki tatu zilizopita.

Shindano hilo kabla ya mchujo, ambalo lilianza majira ya saa 12:30 jioni, liliendeshwa wazi na watangazaji watatu, ambao ni Martina Abera, Davy-Carmel na Luckman Nzeyimana. Kabla ya uteuzi huo washiriki wote na timu ya waandaaji walifanyiwa vipimo vya Covid-19.

Wote hawakukutwa na ugonjwa huo kabla ya kwenda katika hoteli ya La Palisse, Nyamata. Baada ya wiki nzima ya kuomba kupigiwa kura na kuwasilisha mipango yao kwa jamii kupitia vyombo vya habari, Laila Kabagema na Sonia Ishimwe walipata tiketi moja kwa moja baada ya kupata kura nyingi zaidi wakati wa mchakato wa kupiga kura uliofanyika Februari 22 hadi Machi 6 kupitia mitandao kwa njia ya SMS.

Warembo waliopenya ni pamoja na Lorita Benita Isaro, Phiona Uwase, Sonia Uwase Kagame, Linda Uwankusi Nkusi, Sandrine Umutoniwase, Witness Umutoni, Leah Umutesi, Larisa Teta, Hense Teta Musana na Nathalie Musango.

Wakati wengine ni pamoja na Morela Kayitare Isheja, Marie-Paul Kayirebwa, Chrissie Karera, Grace Ingabire, Esther Ingabire, Evelyne Gaju, Hope Akaliza na Amanda Akaliza.

Wakati huohuo, washiriki 17 walitemwa kutoka katika shindano hilo na mara moja waliondolewa katika kambi hiyo na kurudi nyumbani. Washiriki watatumia wiki mbili katika kambi hadi mshindi atakapotangazwa wakati wa fainali itakayofanyika Machi 20. Atachukua taji kutoka kwa Miss Rwanda wa sas

Chanzo: www.habarileo.co.tz