0

Zulfa Macho amchapa Mzambia

Zulfa Macho amchapa Mzambia

Sat, 14 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By Mwandishi wetuDar es Salaam. Bondia Zulfa Macho ameanza vyema katika ngumi za kulipwa baada ya kushinda kwa pointi dhidi ya Alice Mbwewe wa Zambia.

Zulfa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga, Simba na timu ya taifa, Yusuph Macho alishinda kwa pointi 59-56 kutoka kwa jaji John Chagu, 58-56 (Ibrahim Kamwe) na 59-55 kutoka kwa jaji Anthon Rutta.

Macho ambaye amejiunga ngumi za kulipwa hivi karibuni, alionyesha uwezo mkubwa katika pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sport chini ya Mkurugenzi Kelvin Twissa.

Mtanzania huyo alisema kuwa ushindi huo umeongeza hamasa katika ngumi za kulipwa nchini na kupania kufanya vizuri zaidi katika mapambano yajayo.

“Hili ni pambano langu la kwanza la kimataifa, nashukuru nimeweza  kutimiza ndoto yangu, mpinzani wangu alikuwa mzuri sana kutokana na uzoefu aliokuwa nao,” alisema Macho.

Kwa upande wake, Mbewe alikubali matokeo hayo na kuahidi kurudiana naye katika siku zijazo

Chanzo: Mwanaspoti