0

Yassin Ustadh wa ndondi afariki dunia

Mon, 7 Sep 2020 Source: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroAliyekuwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini ((TPBO), Yassin Abdallah 'Ustadh' amefariki dunia leo Septemba 7, 2020 asubuhi jijini Dar es Salaam.

Ustadh aliongoza wakati mchezo huo ukiongozwa chini ya vyama vingi.

Mwili wa Ustadh utazikwa kesho Septemba 8 saa 7 mchana kwenye makaburi ya Buza, Dar es Salaam.

Mdogo wa marehemu, Salehe Mwaipaya amesema ndugu yao amefariki ghafla leo.

"Alikuwa mgonjwa akisumbuliwa na moyo, lakini alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

"Jana nimezungumza naye alikuwa vizuri, lakini ghafla akabadirika na kupoteza maisha leo saa 5 asubuhi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz