0

Yanga SC yamsimamisha kazi Katibu Mkuu

BA0954E0 1A68 4951 B1DD 1A4AC3C9AEC1.jpeg Yanga SC yamsimamisha kazi Katibu Mkuu

Wed, 18 Nov 2020 Source: Millard Ayo

Kamati ya utendaji ya Yanga SC imemsimamisha kazi kaimu katibu mkuu wao na Mkurugenzi wa sheria na wanachama wakili Patrick Simon ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Bado haijawekwa wazi moja kwa moja ni tuhuma zipi hasa zinamkabili wakili Patrick lakini Inaaminika kuwa ni miongoni mwa zile zinazotolewa na kocha wa zamani wa timu hiyo Mwinyi Zahera.

Hivi karibuni video ya Zahera ilisambaa na kumtuhumu kuwa wakili Patrick amekuwa akitoa majibu sio mazuri kwa FIFA kitu ambacho kinaweza kuigharimu Yanga, inasemekana Zahera bado anaidai Yanga na kesi iko FIFA.

Chanzo: Millard Ayo