0

Wamepiga Derby za kutosha

Fri, 6 Nov 2020 Source: mwanaspoti.co.tz

By MWANAHIBA RICHARD SIMBA na Yanga ndiyo klabu kongwe zaidi nchini kwenye Ligi Kuu Bara na zina zaidi ya miaka 80 kwenye soka tangu kuanzishwa. Pia, ndiyo timu ambazo zimekutana mara nyingi zaidi katika ligi.

Msimu huu wa Ligi Kuu Bara, timu hizo zilipangwa kucheza Oktoba 18, lakini kutokana na mwingiliano wa ratiba ya FIFA ambapo timu za Taifa zilikuwa na mechi ya kirafiki, Bodi ya Ligi ililazimika kufanya mabadiliko ambapo sasa zitakutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Ingawa zimekutana mara nyingi lakini kuanzia miaka ya 2000 hadi sasa kuna wachezaji ambao, wamepiga Kariakoo Derby za kutosha tu.

Ukiachana na wale ambao wamekaa na timu hizo pengine kwa misimu mitatu, lakini kuna wale waliokaa na kucheza derby kwa zaidi ya miaka mitano.

Mwanaspoti inakuleta nyota hao wa timu zote mbili ambao wamepiga Karaikoo Derby za kutosha tangu walipojiunga nazo.

MKUDE- SIMBA

Chanzo: mwanaspoti.co.tz