0

Wababe wa Yanga, kumsajili Balotelli

Wababe wa Yanga, kumsajili Balotelli

Thu, 12 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By THOBIAS SEBASTIANNOVEMBA 3, 2019 ulikuwa usiku mbaya kwa mashabiki wa Yanga na wapenzi wa soka Tanzania baada ya kuona timu hiyo ikilala kwa kufungwa mabao 3-0 na kutolewa na wenyeji, Pyramids FC katika mechi iliyochezwa mjini Cairo, Misri kwenye Uwanja wa 30 JUNE.

Mchezo huo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, Yanga ilitolewa kwa kipigo cha jumla cha 5-1 kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza mjini Mwanza.

Taarifa kutoka mtandaoni zinaeleza wababe hao wa Yanga ambao kwa sasa ni miamba ya soka Afrika kutokana na uwekezaji wa pesa walioufanya wameingia katika vita ya kutaka kumsajili straika wa  Brescia inayoshiriki ligi ya serie B, Muitaliano Mario Balotelli (30).

Balotelli ambaye amewahi kupita katika timu kubwa mbalimbali za  Inter Milan, Manchester City, Liverpool, AC Milan, Nice, Olympique de Marseille amekuwa akihusishwa na Pyramids ambao wamekuwa wakimwaga mkwanja wa kutosha katika wachezaji ambao wanasajiliwa kwenye kikosi hiko.

Pyramids katika kuonyesha kuwa wamedhamilia kufanya vizuri na wamefanya uwezekezaji wa pesa za kutosha Septemba 7 mwaka huu, wamemsajili aliyekuwa winga wa Huddersfield Town iliyokuwa Ligi Kuu ya England, Ramadan Sobhi kwa pesa isiyokuwa chini ya Sh8 Bilioni.

Sobhi kabla ya kutua Pyramids kwa mkwanja huo amewahi kucheza timu nyingine kubwa, Al Ahly ya Misri, Stoke City, Huddersfield Town zote za Ligi Kuu ya England na nyinginezo nyingi.  

Chanzo: Mwanaspoti