0

TFF yaziomba klabu Wasifu, Vyeti vya makocha

TFF yaziomba klabu Wasifu, Vyeti vya makocha

Thu, 10 Sep 2020 Source: Dar24

Klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21 zimetakiwa kuwasilisha wasifu na vyeti vya makocha wao.

Ombi hilo kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, limetolewa na Shirikisho la soka nchini TFF, leo Septemba 10, kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino inyoongozwa na Cliford Ndimbo.

Ndimbo amezungumza na waandishi wa habari leo mchana na kusema klabu za Ligi Kuu Bara, zinapaswa kuwasilisha TFF wasifu na vyeti vya makocha wakuu, Makocha wasaidizi, Makocha wa viungo na Makocha wa makipa.

Shiboub kucheza Ligi kuu AlgeriaAmesema mwisho wa kuwasilisha wasifu na vyeti Septemba 15, 2020 na vitu hivyo vinatakiwa kukabidhiwa  kwa mkurugenzi wa ufundi TFF Oscar Mirambo.

Simba SC waifuata Mtibwa Sugar kwa hasira – PichaTamko hilo limetolewa ikiwa na lengo la kuzikumbusha klabu kutekeleza kanuni na sheria za TFF kukusanya taarifa za viongozi na makocha wa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu.

Chanzo: Dar24