0

TFF kuwapa zaidi nafasi wanawake

TFF kuwapa zaidi nafasi wanawake

Fri, 6 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By Saddam SadickSHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limesema ili kuhakikisha wanakuwa na ongezeko la viongozi katika taasisi za mpira hususani kwa wanawake nchini wataendelea kutoa mafunzo kwa lengo la kuwajengea uwezo.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 6 jijini hapa wakati wa hitimisho la kozi ya uongozi na utawala kwa wanawake wa soka, Mkufunzi kutoka kwenye Shirikisho hilo, Henry Tandau kwa sasa wametoa mafunzo ya awali.

Tandau amefafanuwa kuwa hawataishia hapo kutoa mafunzo hayo isipokuwa wataendelea kuwajengea uzoefu hadi ngazi za juu kwa wale watakaofuzu.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo ambayo yalidumu kwa siku tano, wameeleza namna walivyopata ujuzi na matarajio yao binafsi ya baadaye na Taifa kwa ujumla.

Frolida Gabriel amesema mafunzo hayo yamewajengea kujiamini kwani wanawake wengi huwa hawajiamini na kwamba itawasaidia zaidi kufanya vizuri hata kwenye jamii.

Pamela Osena kutoka mkoani Mara amesema mafunzo hayo yatawasaidia kama wanawake lakini hata vijana walio chini ya miaka 14 na kwamba wamejifunza mambo mengi ikiwamo uongozi na masuala ya fedha

Chanzo: Mwanaspoti