0

Stars yapiga kambi Uturuki, kujiandaa na Tunisia

Stars yapiga kambi Uturuki, kujiandaa na Tunisia

Sun, 8 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By OLIPA ASSATIMU ya Taifa ya Tanzania  'Taifa Stars' leo Jumapili, Novemba 8, 2020 imeondoka nchini kwenda Istanbul Uturuki, kuweka  kambi  ya  kujiandaa na mechi na Tunsia ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON), zitakazopigwa 2021.

Stars inacheza na Tunisia Novemba 13 ugenini, wakati mechi ya marudiano itapigwa Tanzania Uwanja wa Benjamin Mkapa, Novemba 17.

Kikosi hicho  chini ya kocha  Etienne Ndayiragije,  kimeondoka  kikiwa na wachezaji wa Simba na Yanga ambao walikuwa na mchezo wa watani wa jadi, uliopigwa jana Jumamosi Novemba 7.

Kuelekea mchezo huo, wadau wa soka wamezungumzia mechi ya Stars na Tunisia kwamba itakuwa na ushindani, huku wakitajwa wachezaji wa Simba na Yanga kwamba watakuwa na msaada mkubwa.

Kocha msaidizi wa Gwambina FC, Athumani Bilali 'Bilo' amesema wachezaji wa Simba na Yanga, wametoka kwenye mechi ngumu ya watani wa jadi, jambo analoona litasaidia kuwa kwenye ari ya mchezo dhidi ya Tunisia.

"Wametoka kwenye mechi ngumu, inayotumia akili nyingi, mbinu, hizo ndizo zitakazowafanya waendelee kuwa kwenye ari ya mchezo na kuwa hamasa kwa wengine ambao hawajatoka kwenye mechi,"amesema Bilali.

Chanzo: Mwanaspoti