0

Siri za ubingwa wa Tanzania Bara

Siri za ubingwa wa Tanzania Bara

Tue, 8 Sep 2020 Source: Mwanaspoti

By MZEE WA UPUPUMpira wa Tanzania kwa asilimia 40 hadi 60 umetawaliwa na mapacha wa Kariakoo, Simba na Yanga.

Asilimia 60 hadi 40 zilizobaki ndizo huangukia kwa timu nyingine kulingana na msimu husika.

Yanga na Simba wanapokuwa katika ubora wao watautawala mpira kwa asilimia 60, halafu wenzangu na mimi waliobaki watanyang’anyana asilimia 40 zilizobaki.

Yanga na Simba wanapokuwa katika ubora wa kawaida watautawala mpira kwa asilimia 50, na asilimia 50 zilizobaki zitaangukia kwa wengine.

Na Yanga na Simba wanapokuwa dhaifu ndipo utawala wao hushuka hadi asilimia 40 na wengine kuchukua zile 60.

Nasema hivyo kwa sababu inategemea na uimara wa ‘jamaa’ hawa katika msimu husika dhidi ya wapinzani wao.

Chanzo: Mwanaspoti